Revelation 16:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mvua kubwa ya mawe yenye uzito wa talanta moja ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mvua yenye mawe makubwa kutoka mbinguni ikawanyeshea watu. Mawe haya yalikuwa na uzito wa kilo 40 kila jiwe. Watu wakamlaani Mungu kwa sababu ya mvua hii ya mawe. Hali hiyo Ilitisha sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mvua kubwa ya mawe, mawe yenye uzito wa talanta moja yakaanguka kutoka mbinguni, yakawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mvua kubwa ya mawe yenye uzito wa talanta moja ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa kama kilo hamsini kila moja, ikawanyeshea watu. Nao wakamtukana Mungu kwa sababu ya mapigo ya mvua hiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa kubwa mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mvua kubwa ya mawe mazito yalinganayo na makonde ikawanyeshea watu toka mbinguni. Lakini watu wakamtukana Mungu kwa ajili ya pigo kuu la mvua ya mawe, kwani pigo lake lilikuwa kubwa mno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mvua ya mawe makubwa yenye uzito wa zaidi ya kilo makumi ine ikanyesha juu ya watu. Nao wakamutukana Mungu kwa sababu ya hilo pigo la mvua ya mawe, kwa maana pigo lile lilileta hasara kubwa sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kuloka mbinguni juu ya wana Adamu. Wana Adamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe. Maana pigo lake kubwa mno.