Revelation 16:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa pili akaimimina bakuli yake baharini. Bahari ikawa kama damu ya mtu aliyekufa. Kila kitu kinachoishi baharini kikafa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo wa pili akalimimina bakuli lake juu ya bahari, ikawa damu, kama damu ya maiti, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha malaika wa pili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawa damu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbe vyote hai baharini vikafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wa pili alipokimwaga chano chake baharini, ndipo, ilipogeuka kuwa damu kama ya mfu; kwa hiyo vikafa mle baharini vyote vilivyokuwamo vyenye uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa pili akamwanga kikombe chake katika bahari. Maji yakageuka na kuwa kama damu ya mufu, na viumbe vyote vyenye uzima vilivyokuwa ndani ya bahari vikakufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa pili akakimimina kichupa chake juu ya bahari, pakawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho va uhayi vikafa katika bahari.