Revelation 16:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema, “Ewe mtakatifu, uliyeko na uliyekuwako! Wewe umetenda sawa kuhukumu mambo hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema: “Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa, wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu, kwa sababu umehukumu hivyo;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo nikasikia malaika wa maji akimwambia Mungu: “Wewe ni yule uliyepo na uliyekuwepo daima. Wewe ni Mtakatifu. Uko sahihi kwa hukumu hizi ulizofanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema, “Ewe mtakatifu, Uliyeko na uliyekuwako! Wewe ni mwenye haki katika hukumu hii uliyotoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema, “Ewe mtakatifu, uliyeko na uliyekuwako! Wewe umetenda sawa kuhukumu mambo hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema: “Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa, wewe uliyeko, uliyekuwako, uliye Mtakatifu, kwa sababu umehukumu hivyo;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema: “Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa, wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu, kwa sababu umehukumu hivyo;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema, “Ewe mtakatifu, uliyeko na uliyekuwako! Wewe umetenda sawa kuhukumu mambo hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikamsikia yule malaika wa maji, akisema: Wewe u mwongofu, uliopo, uliyekuwapo, unatakata, kwa kuwa umehukumu hivyo:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikasikia malaika anayekuwa na uwezo wa kuamuru maji akisema: “Ewe Mutakatifu unayekuwa na uliyekuwa, wewe unahukumu kufuatana na haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, ee Bwana, ulioko, uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivu;