Revelation 16:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa nne akaimimina bakuli yake juu ya jua. Jua lilipewa nguvu kuwachoma watu kwa moto.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo wa nne akalimimina bakuli lake juu ya jua, nalo likaruhusiwa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lake juu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watu kwa moto wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wa nne alipokimwaga chano chake juani, ndipo, lilipopewa kuwaunguza watu kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa ine akamwanga kikombe chake juu ya jua, nalo likapewa uwezo wa kuwaunguza watu kwa joto lake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa nne akakimimina kichupa chake juu ya jua; likapewa kuwaunguza wana Adamu kwa moto.