Revelation 17:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikakumbwa na Roho mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yule malaika akanichukua katika Roho wa Mungu, akanipeleka jangwani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha malaika akanichukua mbali kwa Roho Mtakatifu mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu. Mnyama alikuwa ameandikwa majina ya kumkufuru Mungu katika mwili wake wote. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikakumbwa na Roho mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka nyikani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka jangwani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akanichukua katika Roho hadi jangwani, nikaona mwanamke akiwa ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya kukufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikakumbwa na Roho mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliponipeleka kiroho nyikani, nikaona mwanamke aliyepanda nyama mwekundu aliyejaa majina yenye matusi, naye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikashikwa na Roho wa Mungu, na malaika akanipeleka katika jangwa. Kule nikaona mwanamuke aliyekuwa akiikaa juu ya nyama mumoja wa ajabu mwekundu aliyeandikwa juu yake majina ya kumutukana Mungu. Nyama yule alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi.