Revelation 17:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Isa. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikatambua kuwa mwanamke alikuwa amelewa. Alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu wa Mungu. Alikuwa amelewa kwa damu ya wale walioshuhudia imani yao katika Yesu Kristo. Nilipomwona mwanamke, nilishangaa sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Yesu. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Isa. Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nilipomwona yule mwanamke, alivyolewa kwa damu za watakatifu na kwa damu za mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu mastaajabu makubwa mno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikaona kwamba yule mwanamuke amelewa kwa damu ya watu wa Mungu na ya watu waliouawa kwa sababu ya ushuhuda wao kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona nikashangaa sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.