Revelation 17:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hapa ndipo penye wito wa akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Unahitaji hekima kulielewa hili. Vichwa saba juu ya mnyama ni milima saba ambako mwanamke amekaa. Pia ni watawala saba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hapa ndipo penye akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hapa ndipo penye wito wa akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, panapotakwa werevu wa kweli: vile vichwa saba ni milima saba, ndiyo, yule mwanamke anayokalia juu; nayo ni wafalme saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hapa inafaa kuwa na akili na hekima. Vile vichwa saba ni milima saba, ambavyo yule mwanamuke anaikaa juu yake. Vile vichwa ni vilevile wafalme saba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule.