Revelation 18:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka kuu na dunia ikaangazwa kwa mng’ao wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Malaika huyu alikuwa na nguvu kuu. Utukufu wa malaika ukaing'arisha dunia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu na dunia ikamulikiwa na mng'ao wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu na dunia ikamulikiwa na mng’ao wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya hayo niliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu, na dunia ikamulikwa na mng'ao wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikaona malaika mwingine, akishuka toka mbinguni mwenye nguvu kuu, nchi ikaangazwa na utukufu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mambo hayo, nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni. Yeye alikuwa na uwezo mukubwa; na dunia yote ilingaa kwa utukufu wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BAADA ya haya nalioua malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu, inchi ikaangazwa kwa utukufu wake.