Revelation 18:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marumaru;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya udi, na vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba, chuma na marumaru,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
dhahabu, fedha, vito, lulu, nguo za kitani safi, nguo za zambarau, hariri na nguo nyekundu, aina zote za mti wa udi, na aina zote za vitu vilivyotengenezwa kutokana na pembe za wanyama, miti ya thamani, shaba, chuma, na marimari.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marmari;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marumaru;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya manukato, vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba nyeusi, chuma na marmar,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya udi, na vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba, chuma na marmar,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bidhaa ya dhahabu, fedha, vito vyenye thamani, lulu, kitani nzuri, nguo ya rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, kila chombo cha pembe, kila chombo cha mti wa thamani nyingi, cha shaba, cha chuma na cha marimari;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hakuna tena wa kununua dhahabu yao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombo vya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe za ndovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chuma na marumaru;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
zile za dhahabu na za fedha na za vito na za ushanga na za nguo na za bafta na za nguo za kifalme na za hariri na za rangi nzuri, tena ile miti yote ya kuvukiza na vyombo vyote vya pembe na vya mpingo na vya shaba na vya chuma na vya mawe meupe sana,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
za zahabu, feza, mawe ya bei kali, ushanga, nguo zilizofumwa na nyuzi zuri pamoja na nguo nzuri za rangi nyekundu nyeusi na nyekundu sana, miti yote yenye kunuka vizuri, vyombo vyote vyenye kutengenezwa na pembe, na vyote vinavyochongwa na miti ya bei kali, na vyombo vyote vya shaba, vya chuma, vya mawe yenye kuchongwa,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bidhaa ya dhahahu, na fedha, na jito lenye thamani, na lulu, na katani, na porfuro, na hariri, na nguo nyekundu; na killa mti wa uudi, na killa chombo cha pembe, na killa chombo cha mti wa thamani nyingi na cha shaba na cha chuma na cha marimari: