Revelation 18:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kupitia kwa mali yake! Katika saa moja tu ameangamizwa!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walirusha mavumbi juu ya vichwa vyao na kulia kwa sauti kuu kuonesha huzuni kuu waliyokuwa nayo. Walisema: “Inatisha! Inatisha sana kwa mji mkuu! Wote waliokuwa na meli baharini walitajirika kwa sababu ya utajiri wake! Lakini umeteketezwa katika saa moja!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, Ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kwa kupitia mali zake! Katika saa moja tu ameangamizwa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kupitia kwa mali zake! Katika saa moja tu ameangamizwa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwa sauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mji ambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirika kutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tu umepoteza kila kitu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakajitupia mavumbi vichwani pao, wakapiga kelele wakilia na kuomboleza na kusema: Mama we! Mama we! Mji huu mkubwa! Katika malimbiko yako ndimo, wote walio na vyombo baharini walimopata mali nyingi! Kwa saa moja umeanguka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia na kufanya kilio, nao walilalamika, wakisema: “Ole! Ole kwa muji ule mukubwa! Wote wanaokuwa na mashua za kufanya uchuuzi juu ya bahari walijitajirisha na mali zake nyingi. Lakini kwa muda wa saa moja tu umebaki mutupu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitoka machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole wake mji ule ulio mkuu, ambao ndani yake wote wenye merikebu katika bahari walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.