Revelation 18:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akapaza sauti kwa nguvu, akisema: “ ‘Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu!’ Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika akapaza sauti akasema: “Ameteketezwa! Mji mkuu Babeli umeteketezwa! Umekuwa nyumba ya mapepo. Mji ule umekuwa najisi. Mji uliojaa kila aina ya ndege najisi. Ni mahali ambapo kila mnyama najisi na anayechukiwa anaishi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akapaaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli uliye Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Babuloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao ya mashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndege wachafu na wa kuchukiza mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akapaza sauti kwa nguvu akisema: Umeanguka! Umeanguka mji mkubwa wa Babeli! Umegeuka kuwa kao la mashetani na ngome ya pepo zote wenye uchafu na ya ndege wabaya wote wachukiwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akalalamika kwa sauti kubwa, akisema: “Umebomoka, umebomoka kabisa ule muji mukubwa Babeli! Sasa umekuwa makao ya mashetani ya kila namna, ya pepo wachafu, na makimbilio ya ndege wote wachafu na wenye kuchukiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akalia kwa nguvu, kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya killa roho mchafu, na ngome ya killa ndege mchafu mwenye kuchukiza;