Revelation 18:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia, akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu, wala hautaonekana tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha malaika mwenye nguvu akainua jiwe kubwa. Jiwe hili lilikuwa kubwa kama jiwe kubwa la kusagia. Malaika akalitupia jiwe baharini na kusema: “Hivyo ndivyo mji mkuu Babeli utakavyotupwa chini. Hautaonekana tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika mmoja mwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia, akalibwaga baharini akisema: Kwa nguvu kama hii mji mkubwa wa Babeli utabwagwa upesi hivyo, usionekane tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha malaika mumoja mwenye uwezo akanyanyua jiwe linalokuwa kama jiwe kubwa la kusagia. Akalitupa katika bahari akisema: “Ni hivi muji mukubwa wa Babeli utakavyotupwa kwa nguvu, nao hautaonekana tena.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na malaika mmoja hodari akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Hivi kwa nguvu nyingi utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana kabisa.