Revelation 18:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yoyote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ee Babeli, muziki wa wapigao vinanda na ala zingine waimbaji na tarumbeta, hautasikika tena ndani yako. Hakuna mfanyakazi afanyaye kazi atakayeonekana ndani yako tena. Sauti ya jiwe la kusagia haitasikika ndani yako tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na sauti za wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yo yote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yoyote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikika ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mwako hamtasikilika tena sauti zao wapigao mazeze na ngoma na filimbi na mabaragumu, wala hamtaonekana tena mwako fundi aliye yote wa kazi yo yote, wala hamtasikilika tena mwako sauti ya kusaga,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sauti ya wapiga vinubi na ya wapiga vinanda, ya wapiga filimbi na ya baragumu, haitasikilika ndani yako tena. Fundi wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena hata kidogo wala kelele la jiwe la kusagia halitasikilika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala sauti ya wapiga vinanda na ya wapiga mazumari na ya wapiga filimbi na ya wapiga baragumu haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi aliye yote wa kazi iliyo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;