Revelation 18:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanga wa taa hautang'aa ndani yako tena. Sauti za maarusi hazitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu wakuu wa ulimwengu. Mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikiwa ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikika ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanga wa taa hautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi na bibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiashara wako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wako mataifa yote yalipotoshwa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wala hamtamulika tena mwako mwanga wa taa, wala sauti ya mchumba wa kiume na wa kike haitasikilika tena mwako. Kwani wachuuzi wako walikuwa wakuu wa nchi, kwani kwa uchawi wako wamizimu wote walipotezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwangaza wa taa hautaonekana tena ndani yako. Na hakutasikilika tena kelele la wenye kuoa au kuolewa. Itakutokea vile kwa sababu wachuuzi wako walikuwa wenye uwezo mukubwa katika dunia, nawe umewadanganya watu wote kwa njia ya vitendo vyako vya uchawi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.