Revelation 18:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake. Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, na wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wote wa dunia wamekunywa mvinyo wa uzinzi wake na ghadhabu ya Mungu. Watawala wa dunia walizini pamoja naye, na wafanya biashara wa ulimwengu walitajirika kutokana na utajiri wa anasa zake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa uasherati wake. Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye, nao wafanya biashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake. Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi nao, nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana mataifa yote yalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiashara wa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizo na kipimo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wamizimu wote wamekunywa mvinyo mkali za ugoni wake, wafalme wa nchini wakafanya ugoni naye, wachuuzi wa nchini wakapata mali nyingi kwa hivyo, alivyokaza kuyatapanya yaliyokuwa yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa sababu mataifa yote yalileweshwa na divai kali ya uasherati wa muji ule. Wafalme wa dunia wamezini nao, na wachuuzi wa dunia wamejitajirisha kutokana na uwingi wa mali zake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.