Revelation 18:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “ ‘Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,’ ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Enyi watu wangu, tokeni katika mji huo, ili msishiriki katika dhambi zake. Ili msiteseke kwa adhabu yoyote kuu atakayoipata.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lo lote;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikasikia sauti nyingine iliyotoka mbinguni kwamba: Enyi mlio watu wangu, tokeni kwake! Maana msiwe wenzake wa makosa yake, wala msipate nanyi mapigo yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikasikia sauti ingine kutoka mbinguni ikisema: “Mutoke katika muji ule ninyi watu wangu, kusudi musishiriki zambi zake na kupatwa vilevile na mapigo yatakayoupata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.