Revelation 18:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, kulingana na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: ‘Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alijipa utukufu mwingi na kuishi kitajiri. Mpeni mateso mengi na huzuni nyingi. Kama vile utukufu na starehe aliyoifurahia. Hujisemea mwenyewe, ‘Mimi ni malkia nikaaye kwenye kiti changu cha enzi. Mimi si mjane; Sitakuwa na huzuni.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, kulingana na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: ‘Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, kulingana na kuishi kwake kwa anasa. Maana anajisemea moyoni: ‘Ninaketi hapa; mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, alivyojitukuza na kuyatapanya yaliyo yake, kazeni vivyo hivyo kumtesa na kumwumiza! Kwa sababu husema moyoni mwake: Nafuliza kuwa mfalme wa kike, nami si mwanamke mjane, wala sitaona masikitiko kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa kadiri ulivyojitukuza na kuishi katika raha, kwa kadiri ile ile muuletee mateso na huzuni. Muji ule unajisemesha: ‘Mimi ninaikaa juu ya kiti cha kifalme kama vile malkia; mimi si mujane, wala sitapata huzuni hata kidogo!’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kadiri aliyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa alisema moyoni mwake, Nimeketi malkiya, nami si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.