Revelation 18:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: Ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ana nguvu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana Mwenyezi Mungu amhukumuye ana nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo katika siku moja atateseka kwa njaa kuu, maombolezo na kifo. Atateketezwa kwa moto, kwa sababu Bwana Mungu anayemhukumu ni mwenye nguvu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ni Mwenye Uwezo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ana nguvu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana amhukumuye ni BWANA Mungu Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu amhukumuye ana nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: Ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ana nguvu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo mapigo yake yatamjia yote siku moja, kufiwa na kusikitika na kuumwa na njaa; kisha atateketezwa kwa moto kabisa. Kwani Bwana Mungu atakayemhukumu ni mwenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo, kwa muda wa siku moja tu utapatwa na mapigo ya mauti, huzuni na njaa. Na zaidi ya hiyo utateketezwa kwa moto, kwa maana Bwana wetu, Mungu anayeuhukumu, ni mwenye uwezo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, manti, na huzuni, na njaa, nae atateketezwa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni hodari.