Revelation 19:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya umati wa watu wengi mbinguni ikisema, “Asifiwe Mungu! Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Mungu wetu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipaza sauti na kusema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya hili nikasikia kitu kilichosikika kama kundi kubwa la watu mbinguni. Walikuwa wakisema: “Haleluya! Ushindi, utukufu na nguvu ni vyake Mungu wetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya umati wa watu wengi mbinguni ikisema, “Haleluya! Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Mungu wetu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya umati wa watu wengi mbinguni ikisema, “Asifiwe Mungu! Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Mungu wetu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; Wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya umati wa watu wengi mbinguni ikisema, “Asifiwe Mungu! Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Mungu wetu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikasikia uvumi mkuu kama wa makundi mengi ya watu waliomo mbinguni, wakisema: Haleluya! Wokovu na utukufu na uwezo ni wa Mungu wetu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; Wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mambo hayo, nikasikia kelele kutoka mbinguni linalosikilika kama vile sauti kubwa ya kundi kubwa la watu ikisema: “Mungu asifiwe! Wokovu, utukufu na uwezo ni vya Mungu wetu. Yeye anastahili utukufu na uwezo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BAADA ya baya nikasikia sauti ya makutano mengi, sauti kubwa katika mbingu, ikisema, Halleluya; Wokofu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu;