Revelation 19:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. Alikuwa na taji nyingi kichwani mwake. Jina lilikuwa limeandikwa juu yake, lakini yeye peke yake ndiye aliyejua maana ya jina hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu ye yote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Macho yake ni moto unaowaka, kichwani pake anavyo vilemba vingi vya kifalme. Analo jina, aliloandikwa; hakuna aliyelijua pasipo yeye mwenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Macho yake yalimetameta kama ndimi za moto, na juu ya kichwa chake kulikuwa taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa juu yake, wala hakuna mutu aliyejua, isipokuwa yeye mwenyewe tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na macho yake yalikuwa kama mwako wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi, nae ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu illa yeye mwenyewe.