Revelation 19:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, naye akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikaona malaika amesimama katika jua. Kwa sauti kuu malaika akawaambia ndege wote wanaoruka angani, “Kusanyikeni kwa ajili ya karamu kuu ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njoni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njooni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikaona malaika mmoja aliyesimama katika jua na kupaza sauti kuu akiwaambia ndege wote warukao mbinguni kati: Njoni, mkusanyikie vyakula vingi vya Mungu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona malaika mumoja amesimama katika jua. Alikuwa akilalamikia ndege wote waliokuwa wakiruka juu katika anga akiwaambia: “Mukuje mukutane pamoja kwa karamu kubwa ya Mungu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaona malaika mmoja amesimama katika jua, akilia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao kati kati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu,