Revelation 19:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki. Amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake. Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hukumu zake ni za kweli na za haki. Mungu wetu amemwadhibu kahaba. Ndiye aliyeiharibu dunia kwa uzinzi wake. Mungu amemwadhibu kahaba kulipa kisasi cha vifo vya watumishi wake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki. Amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake. Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa maana hukumu zake ni za kweli na za haki. Amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake. Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki. Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwa ameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibu kwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani hukumu zake ni za kweli na za wongofu. Kwani amemhukumu yule mgoni mkuu wa kike aliyeiangamiza nchi kwa ugoni wake, akamlipiza damu za watumwa wake waliouawa na mkono wake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hukumu zake ni za kweli na za haki. Amehukumu yule kahaba mukubwa ambaye alikuwa akipotosha dunia kwa vitendo vyake vya uasherati. Mungu amemulipiza kisasi cha damu ya watumishi wake!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake.