Revelation 19:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: “Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sauti ikatoka kwenye kiti cha enzi na kusema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi nyote mnaomtumikia! Msifuni Mungu wetu, ninyi nyote mlio wadogo na wakubwa mnaomheshimu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: “Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: “Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, kukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: “Msifuni Mungu enyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauti ikatoka kitini mwa kifalme ikisema: Mvumisheni Mungu wetu, enyi watumwa wake nyote mnaomwogopa yeye, mlio wadogo na wakubwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha sauti ikasikilika toka kwenye kiti cha kifalme ikasema: “Mumusifu Mungu wetu ninyi watumishi wake wote, ninyi wote munaomuheshimu, wakubwa na wadogo!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sauti ikatoka katika kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo na wakuu.