Revelation 19:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumo kubwa, ikisema, “Asifiwe Mungu! Maana Bwana Mungu wetu Mwenye Nguvu ametawala!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipaza sauti na kusema: “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikasikia kitu kilichosikika kama kundi kubwa la watu. Kilikuwa na kelele kama mawimbi ya bahari au radi. Watu walikuwa wakisema: “Haleluya! Bwana Mungu wetu anatawala. Ndiye Mwenye Nguvu, Mungu Mwenyezi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumo kubwa, ikisema, “Haleluya! Maana Bwana Mungu wetu Mwenye Uwezo ni Mfalme!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumo kubwa, ikisema, “Asifiwe Mungu! Maana Bwana Mungu wetu Mwenye Nguvu ametawala!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana BWANA Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema: “Haleluya! Kwa maana bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umati mkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumo kubwa, ikisema, “Asifiwe Mungu! Maana Bwana Mungu wetu Mwenye Nguvu ametawala!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasikia uvumi kama wa makundi mengi na kama uvumi wa maji mengi na kama uvumi wa ngurumo yenye nguvu wa kwamba: Haleluya! Kwani mfalme ni Bwana Mungu wetu aliye Mwenyezi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikasikia sauti inayosikilika kama kelele la kundi kubwa la watu, na kama ngurumo ya maporomoko ya maji mengi na kama ngurumo kubwa ya radi ikisema: “Mungu asifiwe! Kwa maana yeye Bwana wetu, Mungu wetu Mwenye Uwezo anatawala.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki.