Revelation 19:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapewa kitani safi, inayong’aa na nzuri, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nguo ya kitani safi ilitolewa kwa bibi arusi ili avae. Kitani ilikuwa safi na angavu.” (Kitani safi inamaanisha mambo mazuri ambayo watakatifu wa Mungu waliyatenda.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watu wa Mungu.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapewa kitani safi, nyeupe inayong'aa, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapewa kitani safi, nyeupe inayong’aa, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing'aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akapewa kuvaa nguo za bafta zing'aazo na kumetuka. Maana hizi nguo za bafta ndio wongofu, watakatifu waliopewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule bibi amepewa nguo ya kuvaa iliyofumwa na nyuzi nzuri zenye kungaa. (Nguo ile ni mufano wa matendo ya haki ya watu wa Mungu.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.