Revelation 2:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi hataumizwa na kifo cha pili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho wa Mungu ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye hatadhuriwa kamwe na mauti ya pili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa. Wale watakaoshinda hawatadhuriwa na mauti ya pili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi hataumizwa na kifo cha pili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa na mauti ya pili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye hatadhuriwa kamwe na mauti ya pili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi hataumizwa na kifo cha pili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule! Mwenye kushinda hatapotolewa na kufa kwa pili.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwenye kuwa na masikio, asikie vizuri vile Roho anavyoambia makanisa! “Yule atakayeshinda hatapatwa na kifo cha pili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.