Revelation 2:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninajua unakoishi: kule Shetani ana kiti chake cha utawala. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu, hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu mkuu, anakoishi Shetani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninapafahamu mahali unapoishi. Unaishi mahali kilipo kiti cha enzi cha Shetani, lakini wewe ni mwaminifu kwangu. Hukukataa kueleza kuhusu imani yako kwangu hata wakati wa Antipa. Antipa alikuwa shahidi wangu mwaminifu aliyeuawa katika mji wako, mji ambao shetani anaishi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambako ndiko anakokaa Shetani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji mkuu wenu, ambako ndiko anakoishi Shetani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninapajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napajua, unapokaa. Ni hapo, kiti cha kifalme cha Satani kilipo. Lakini unalishika sana Jina langu, hukukana, ya kuwa unanitegemea mimi, hata siku zile, shahidi wangu mwelekevu Antipa alipouawa huko kwenu, Satani anakokaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninajua pahali pale unapokaa, ile ndiyo nafasi ya utawala wa Shetani. Wewe unashikamana na jina langu, wala haukuikana imani unayokuwa nayo kwangu, hata wakati Antipa, mushuhuda wangu mwaminifu, alipouawa kati yenu kule kwenye makao ya Shetani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.