Revelation 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho wa Mungu ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa! Kila atakayeshinda nitampa mana iliyofichwa. Pia nitampa kila mshindi jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu yake. Na hakuna atakayejua jina hili isipokuwa yule atakayepata jiwe hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa yeye jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye masikio na asikie, Roho anavyowaambia wateule! Mwenye kushinda nitamgawia ile Mana iliyofichwa, kisha nitampa kijiwe cheupe, namo katika kijiwe hiki limeandikwa jina jipya lisilojulika kwa mtu, asipokuwa mwenye kulipata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwenye kuwa na masikio, asikie vizuri vile Roho anavyoyaambia makanisa! “Yule atakayeshinda, nitamupa ile mana iliyofichwa. Na nitamupa vilevile jiwe dogo jeupe, na juu yake kumeandikwa jina jipya ambalo hakuna mutu yeyote anayelijua, isipokuwa tu yule anayelipewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.