Revelation 2:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nayajua matendo yako, upendo wako na imani yako, huduma na saburi yako, na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninayajua matendo yako. Ninajua kuhusu upendo wako, imani yako, huduma yako na uvumilivu wako. Ninajua kwamba unafanya zaidi sasa kuliko ulivyofanya kwanza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na saburi yako na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nayajua matendo yako, upendo wako na imani yako, huduma na saburi yako, na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayajua matendo yako ya kupenda na ya kumtegemea Mungu na ya kutumikia na ya kuvumilia kwako. Tena najua: kazi zako za mwisho ni nyingi kuliko za kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninajua matendo yako, upendo wako, imani yako, kazi yako na uvumilivu wako. Ninajua kwamba sasa unajitolea kwa kunitumikia kuliko mbele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.