Revelation 2:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nitawaua watoto wake. Nayo makundi yote ya waumini yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, nitawaua wafuasi wake. Ndipo makanisa yote wataona kuwa mimi ndiye ninayefahamu kile ambacho watu wanadhani na kufikiri. Na nitamlipa kila mmoja wenu kutokana na kile alichotenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nitawaua watoto wake. Nayo makundi yote ya waumini yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata watoto wake nitawaua, wafe. Ndipo, wateule wote watakaponitambua, ya kuwa mimi ni mwenye kuyapeleleza mafigo, hata mioyo. Nami nitawapa ninyi kila mmoja, kama matendo yenu yalivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaua wafuasi wake. Na hivi makanisa yote yatajua kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo ya watu na mafikiri yao. Vilevile yatajua kwamba mimi nitamulipa kila mumoja wenu kufuatana na matendo yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.