Revelation 20:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iwapo mtu yeyote jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na yeyote ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa kwenye kitabu cha uzima alitupwa kwenye ziwa la moto.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu asipoonekana, ya kuwa ameandikwa katika kitabu cha uzima, akatupwa ziwani mwenye moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mutu yeyote ambaye jina lake lililokosa kuandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.