Revelation 20:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika akalitupa kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka 1,000 itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamtupa katika lile Shimo, akamfunga humo na kulitia muhuri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa hadi hiyo miaka elfu itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akamtupia kuzimu na akaifunga. Malaika akamfungia joka kuzimu ili asiweze kuwadanganya watu wa dunia mpaka miaka elfu moja iishe. Baada ya miaka elfu moja joka lazima aachiwe huru kwa muda mfupi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika akalitupa Kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika akalitupa kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka 1,000 itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamtupa katika lile Shimo lisilo na mwisho, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamtupa katika lile Shimo, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika akalitupa kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka 1,000 itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamtupa kuzimuni, akamfungia lango, akatia muhuri juu yake, kusudi asiwadanganye wamizimu tena, mpaka ile miaka elfu imalizike. Itakapokwisha kutimia, sharti afunguliwe siku kidogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika yule akamutupa ndani ya shimo ndefu la kuzimu. Akalifunga na kutia kitambulisho cha muhuri juu yake kwamba lisifunguliwe kusudi nyoka yule asiyadanganye tena mataifa mpaka ile miaka elfu moja ipate kutimia. Kisha miaka hiyo, anapaswa kufunguliwa tena kwa muda mufupi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akamtupa katika abuso, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hatta ile miaka elfu itimie; na baada ya haya imepasa afunguliwe muaa mchache.