Revelation 20:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Atatoka na kwenda kuwadanganya mataifa katika dunia yote, mataifa yajulikanayo kama Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya watu kwa ajili ya vita. Kutakuwa watu wengi wasiohesabika kama mchanga katika ufukwe wa bahari.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko Pwani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za dunia, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, atakapotoka kuwadanganya wamizimu walioko katika pembe nne za nchi, ni wale wa Gogi na wa Magogi, awakusanye kupiga vita, nao watakuwa wengi kama mchanga wa ufukoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
naye atakwenda kuwadanganya watu wa mataifa wanaokuwa katika pande zote za dunia, ndio wanaoitwa Gogi na Magogi. Shetani atawakusanya kwa kupigana vita, nao watakuwa wengi kama vile muchanga wa bahari.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nae atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za inchi, Gog na Magog, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.