Revelation 21:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akanichukua katika Roho wa Mungu hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika akanichukua kwa Roho Mtakatifu mpaka kwenye mlima mkubwa na mrefu. Akanionyesha mji mtakatifu wa Yerusalemu. Mji ulikuwa ukiteremka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionyesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, likishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akanichukua katika Roho mpaka katika mlima mkubwa, mrefu, akanionesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akanichukua kiroho, akanipeleka juu ya mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu wa Yerusalemu ushukao toka mbinguni kwake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikashikwa na Roho, na malaika akanipeleka juu ya mulima mukubwa na murefu. Akanionyesha muji mutakatifu, ndio Yerusalema uliokuwa ukishuka toka mbinguni kwa Mungu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu,