Revelation 21:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mji ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mbili. Kulikuwa malaika kumi na mbili kwenye milango. Kwenye kila mlango kuliandikwa jina la kabila moja la Israeli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na malaika wanangojea kumi na wawili. Majina ya wangoja milango kumi na mawili ya Israeli yalikuwa yameandikwa juu ya milango hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya makabila kumi na mawili ya Waisraeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulikuwa na boma ya mawe kubwa na refu, lililokuwa na malango kumi na mawili, napo malangoni juu palikuwa na malaika kumi na wawili. Hata majina yalikuwa yameandikwa humo malangoni, ndiyo yale ya mashina kumi na mawili ya wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulikuwa ukizungukwa na ukuta mukubwa na murefu wenye milango kumi na miwili na wamalaika kumi na wawili walichunga milango ile. Na juu ya milango ile, kulikuwa kumeandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya Waisraeli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ulikuwa ua ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango thenashara, na katika ile milango malaika thenashara, na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila thenashara za wana wa Israeli.