Revelation 21:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya kila jiwe palikuwa pameandikwa mojawapo ya majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na mbili, na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuta za mji zilijengwa kwenye mawe kumi na mbili ya msingi. Kwenye mawe kulikuwa kumeandikwa majina ya mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya mawe hayo yalikuwa yameandikwa majina na mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya kila jiwe palikuwa pameandikwa mojawapo ya majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi kulikuwa na majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-kondoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya kila jiwe palikuwa pameandikwa mojawapo ya majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hilo boma la mji lilikuwa lenye misingi kumi na miwili, namo misingini mlikuwamo majina kumi na mawili, ni ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana kondoo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ukuta uliozunguka muji ule ulikuwa umejengwa juu ya mawe ya musingi kumi na mawili na juu ya kila jiwe kulikuwa kumeandikwa jina la kila mumoja wa mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo.