Revelation 21:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: Ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama stadioni 12,000; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mji ulijengwa kimraba. Urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Malaika aliupima mji kwa fimbo. Mji ulikuwa na urefu wa kilomita 2,400, upana wake ulikuwa kilomita 2,400, na kimo chake kwenda juu kilikuwa kilomita 2,400.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa na urefu, upana na urefu wa kwenda juu, kama kilomita elfu mbili na mia nne.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,400; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu moja na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: Ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huo mji ulikuwa umejengwa kwenye pembe nne, urefu wake ni sawa na upana wake; akaupima mji kwa ule mwanzi, ukawa kama mwendo wa siku za mchana mia nne. Urefu wake na upana wake nao urefu wake wa juu ni sawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muji ule ulikuwa umejengwa namna ya muraba, urefu wake na upana wake vilikuwa sawasawa. Malaika akapima muji ule na ile fimbo; ulikuwa na urefu, upana na urefu wake wa kwenda juu yapata kilometre elfu mbili na mia ine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ule mji ni wa mrabba, na marefu yake sawa sawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi, hatta stadio thenashara elfu. Marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake mamoja.