Revelation 21:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikauona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukiteremka kutoka mbinguni kwa Mungu. Ulikuwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyevalishwa kwa ajili ya mumewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikauona mji mtakatifu wa Yerusalemu mpya, ukishuka toka mbinguni kwake Mungu. Ulikuwa umetengenezwa kama mchumba mke aliyepambiwa mumewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikaona muji mutakatifu, ndio Yerusalema mupya, uliokuwa ukishuka toka mbinguni kwa Mungu, nao ukitengenezwa vizuri kama vile bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya kwenda kukutana na mume wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.