Revelation 21:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikasikia sauti kuu kutoka kwenye kiti cha enzi. Ikisema, “Makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu. Yeye ataishi pamoja nao. Na wao watakuwa watu wake. Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao naye atakuwa Mungu wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Mungu amefanya makao yake kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasikia sauti kuu iliyotoka kitini mwa kifalme, ikisema: Tazama, kituo chake Mungu cha kukaa pamoja na watu! Humo atatua pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu atakuwa pamoja nao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikasikia sauti kubwa tokea kwenye kiti cha kifalme ikisema: “Sasa makao ya Mungu yanapatikana kati ya watu! Yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atakuwa Mungu wao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao.