Revelation 21:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yoyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akaniambia, “Imekwisha! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Kila mwenye kiu nitampa bure maji kutoka kwenye chemichemi ya maji ya uzima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yoyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Yamekwisha kufanyika. Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na mwisho. Aonaye kiu, mimi nitampa bure ya kunywa toka kisimani mwenye maji ya uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akasema tena: “Sasa ni mwisho! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Yule anayesikia kiu, nitamupa maji ya kunywa yanayotoka katika chemichemi ya maji ya uzima pasipo kulipa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.