Revelation 22:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Heri walioosha kanzu zao. Watakuwa na haki ya kula chakula kutoka kwenye mti wa uzima. Wanaweza kuingia katika mji kwa kupitia katika malango yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, kwani watakuwa na haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye shangwe ndio waliozifua nguo zao, wapewe kuufikia mti wa uzima na kuingia malangoni mwa ule mji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Heri wale wanaosafisha kanzu zao, kwa maana watakuwa na haki ya kukula matunda ya muti wa uzima na ya kuingia katika muji ule kwa kupitia kwenye milango.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.