Revelation 22:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi, Isa, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya jumuiya ya waumini. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi inayong’aa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kukuambia mambo hayo kwa ajili ya makanisa. Mimi ni mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi ing'aayo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi, Isa, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya jumuiya ya waumini. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi ing’aayo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu, awashuhudie haya penye wateule. Mimi ni mzizi na mzao wa Dawidi, ile nyota imulikayo mapema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mimi Yesu, nimemutuma malaika wangu kwa kuwashuhudia maneno haya yote katika kanisa. Mimi ni wa shina na wa uzao wa mufalme Daudi. Mimi ni nyota ya asubui.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.