Revelation 22:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hutiririka kupitia katika mtaa mkuu wa mji. Mti wa uzima uko kila upande wa mto, na huzaa tunda kila mwezi, mara kumi na mbili kwa mwaka. Majani ya mti ni kwa ajili ya kutibu mataifa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uwanjani katikati na kandokando ya mto pande zote mbili kulikuwa na miti ya uzima izaayo matunda mara kumi na mbili, kila mwezi hutoa matunda yao, nayo majani ya miti ndiyo yanayowapa wamizimu uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muto ule ulitelemuka katikati ya barabara ya muji mutakatifu. Kandokando ya ule muto, kulikuwa kumeota muti wa uzima, nao unatoa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, maana yake mara moja kila mwezi. Majani ya muti ule yanatumiwa kama dawa ya kuponyesha mataifa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kati ya njia kuu yake na ule mto, upande huu na upande huu, mti wa uzima, uzaao matunda thenashara, mwenye kutoa matunda yake killa mwezi, na majani ya mti huo ya kuwaponya mataifa.