Revelation 22:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Mwenyezi Mungu, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminiwa. Bwana, Mungu awavuviaye manabii, amemtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee hivi karibuni:
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. BWANA, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. bwana Mwenyezi, aliye Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaniambia: Maneno haya yapasa kutegemewa, maana ni ya kweli, naye Bwana Mungu wa roho za wafumbuaji amemtuma malaika wake, awaonyeshe watumwa wake yatakayofanyika upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha yule malaika akaniambia: “Maneno haya ni ya kweli na ya uhakika. Na Bwana Mungu anayewaongoza manabii kwa njia ya Roho wake ametuma malaika wake kwa kuwaonyesha watumishi wake mambo yanayopaswa kutokea kisha kidogo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.