Revelation 3:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Sardi, andika: Haya ndio maneno ya aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Andika hivi kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi: Huu ni ujumbe kutoka kwake Yeye mwenye roho saba na nyota saba. Ninayajua matendo yako. Watu husema kuwa u hai, lakini hakika umekufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika hivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye na roho saba za Mungu na nyota saba. Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Sardi andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Sardi, andika: “Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Malaika wa wateule walioko Sarde mwandikie: Ndivyo anavyosema yeye aliye mwenye zile roho saba za Mungu na mwenye zile nyota saba. Nayajua matendo yako, unalo jina la kuwa unaishi, lakini u mfu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Umwandikie malaika wa kanisa la Sardi hivi: “Ujumbe huu unatoka kwa yule anayekuwa na roho zile saba za Mungu na zile nyota saba. Ninajua matendo yako, hakika wewe umekwisha kufa ingawa unajulikana kuwa muzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.