Revelation 3:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Amka! Jitie nguvu kabla ya nguvu kidogo uliyonayo haijakuishia kabisa. Unachofanya hakistahili kwa Mungu wangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyobakia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amka, uyashupaze masao yanayotaka kufa nayo! Kwani sikuyaona matendo yako, ya kuwa yametimilika mbele ya Mungu wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amuka! Uimarishe kile kinachobaki kinachokaribia kufa, kwa maana nimeona kwamba matendo yako si makamilifu mbele ya Mungu wangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe manibo yaliyosalia, yaliyo tayari kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu.