Revelation 3:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe sivyo, ila wanasema uongo. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako, wapate kujua kwamba nimekupenda wewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, nitawafanya waje wapige magoti miguuni pako, na wakiri kwamba nimekupenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sikiliza! Kuna kundi la Shetani. Wanasema kuwa wao ni Wayahudi, lakini ni waongo. Si Wayahudi halisi. Nitawafanya waje mbele yako na kusujudu kwenye miguu yako. Watajua ya kuwa ninakupenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe ni wadanganyifu. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako wapate kujua kwamba kweli nakupenda wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe sivyo, ila wanasema uongo. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako, wapate kujua kwamba nimekupenda wewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watatambua ya kwamba nimekupenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, nitawafanya waje wapige magoti miguuni pako, na wakiri ya kwamba nimekupenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe sivyo, ila wanasema uongo. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako, wapate kujua kwamba nimekupenda wewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, nitakupa wanafunzi wa Satani wanaojisema kuwa Wayuda, lakini sio, ila husema uwongo. Tazama, nitawaleta hao, waje, wakuangukie penye miguu yako, watambue, ya kuwa mimi nimekupenda wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia, nitakupa watu wa kikundi chenye kuabudu Shetani, ndio wale wasema uongo wanaojidai kwamba wao ni Wayuda, lakini ni wadanganyifu. Hakika nitawalazimisha kupiga magoti mbele yako, nao watajua ya kuwa mimi ninakupenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tazama, nakupa walio wa sunagogi la Shetani, wasemao kwamba wao ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uwongo. Tazama, nitawafanya waje wasujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupeuda.