Revelation 4:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango uliokuwa wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo mwanzo ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo huku, nami nitakuonesha yale ambayo hayana budi kutendeka baada ya haya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikatazama, na mbele yangu ulikuwepo mlango uliokuwa wazi mbinguni. Na nikasikia sauti iliyosema nami mwanzoni. Ilikuwa sauti iliyosikika kama tarumbeta. Ilisema, “Njoo huku juu, nitakuonesha yale ambayo ni lazima yatokee baada ya hili.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu nami nitakuonyesha mambo yatakayotukia baadaye.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango ulio wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo kwanza ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo panda huku nami nitakuonyesha yale ambayo hayana budi kutokea baada ya haya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango uliokuwa wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo mwanzo ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo, huku, nami nitakuonyesha yale ambayo hayana budi kutokea baada ya haya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya hayo niliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nalitazama, nikaona mlango mbinguni uliokuwa wazi. Ndipo, sauti ile ya kwanza, niliyoisikia kama ya baragumu, iliyosema nami, iliposema: Panda huku, nikuonyeshe yatakayofanyika, haya yakiisha! Papo hapo nikawapo kiroho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya mambo hayo nilipata maono mengine. Niliona mulango mumoja umefunguliwa wazi mbinguni. Halafu ile sauti niliyosikia mara ya kwanza, iliyolia kama baragumu, ikaniambia: “Panda huku, nami nitakuonyesha mambo yanayopaswa kutokea nyuma ya hayo ya mbele.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.