Revelation 4:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake aliyeketi kwenye kiti cha enzi, na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi, wakisema:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
wazee ishirini na nne waliinama mbele ya yule anayekaa kwenye kiti cha enzi. Wanamwabudu anayeishi milele na milele. Wanaweka taji zao mbele ya kiti cha enzi na kusema:
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi, wakisema:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake aketiye kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi, wakisema:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, wale wazee 24 walipomwangukia yule aliyekaa kitini mwa kifalme na kumtambikia yeye aliye mwenye kuwapo kale na kale pasipo mwisho; wakavitupa vilemba vyao mbele ya kiti cha kifalme wakisema:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wale wazee makumi mbili na wane waliinama uso mpaka chini mbele ya yule anayeikaa juu ya kiti cha kifalme, wakimwabudu huyo anayeishi kwa milele na milele. Nao walikuwa wakikuja kuweka taji zao mbele ya kiti chake, na kusema:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,