Revelation 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wastahili ee Bwana na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako viliumbwa na vipo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Bwana wetu na Mungu! Unastahili kupokea utukufu, heshima na nguvu. Uliumba vitu vyote. Kila kinachoishi kiliumbwa kwa sababu ulitaka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufu na heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako kila kitu kimepewa uhai na uzima.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wastahili ee Bwana na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako viliumbwa na vipo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako viliumbwa na vimekuwako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wastahili ee Bwana na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako viliumbwa na vipo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana na Mungu wetu, umepaswa na kupewa utukufu na heshima na uwezo, kwani wewe uliviumba vyote; kwa hayo, uyatakayo, vikapata kuwapo vilipokwisha kuumbwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili utukufu, heshima na uwezo, kwa maana wewe ndiwe uliyeumba vitu vyote; vile vimeumbwa na kupata kuwa kutokana na mapenzi yako.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.